• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tumaini, Isiolo Starlets mibabe wa Chapa Dimba Mashariki

  (GMT+08:00) 2020-02-14 17:04:37

  Tumaini School FC na Isiolo Starlets zimetangazwa mafahali na malkia wa Chapa Dimba na Safaricon Season Three, katika Mkoa wa Mashariki nchini Kenya baada ya kunyamazisha wapinzani wao katika fainali zilizopigiwa Kenyatta Stadium, Machakos. Tumaini ya Makueni iliichapa Black Panthers ya Meru mabao 4-1 katika fainali ya kusisimua. Nayo Isiolo Starlets iliibuka wakali mbele ya Chuka University ilipoilaza mabao 3-2. Fainali ya wavulana ilianza kwa kasi ambapo Tumaini ilijipatia bao la kwanza kunako dakika ya nne lililopachikwa kimiani na Yasin Mohamed, kabla ya kuongeza mabao mawili dakika ya 19 na 47 na kutinga 'hat trick.' Hata hivyo wachezaji wa Black Panthers walionyesha kwamba wao sio mende ambapo walijitahidi kwa udi na uvumba na kufunga bao la kufuta machozi lililopachikwa kimiani na Enow Abdumalik dakika ya 83. Dakika tano baadaye Tumaini iliongezea bao la nne na la kufunga shughuli lililojazwa kimiani na Kapirante Moris.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako