Maambukizi ya virusi vipya vya korona COVID-19 ni changamoto kubwa inayokabili China, na Wachina wameshikamana kwa karibu kupambana na maambukizi hayo.
Mji wa Wuhan ni kitovu cha maambukizi ya korona (COVID-19) nchini China. Takwimu zilizotolewa na Kamati Kuu ya Afya ya China zinaonyesha kuwa, mpaka terehe 12, zaidi ya asilimia 57 ya watu walioambukizwa wanatoka mji huo. Tarehe 23 mwezi uliopita, mji wa Wuhan ulifunga njia zote za kutoka na kuingia, ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya korona katika sehemu nyingine. Baadaye, miji mingine yenye maambukizi mkoani Hubei ikiwemo Ezhou, Xiantao, Qianjiang, Huanggang na Jingmen pia ilifunga njia za kutoka na kuingia. Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Ghebreyesus ameipongeza hatua hiyo ya China akisema, itapunguza maambukizi, na kufanya athari ya maambukizi hayo iwe chini zaidi duniani. Zaidi ya hayo, mji wa Wuhan umejenga hospitali mbili kubwa za maambukizi kwa zaidi ya siku kumi tu.
Wakati wakazi wa mkoa wa Hubei wanapopambana na maambukizi, sehemu nyingine za China zimetoa misaada mbalimbali inayohitajika. Hadi tarehe 13 mwezi huu, zimetuma madaktari zaidi ya elfu 20 kwa mkoa wa Hubei, haswa mji wa Wuhan. Licha ya hayo, pia zimetoa vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi na matibabu.
Rais Xi Jinping wa China alipokagua kazi za kupambana na maambukizi mjini Beijing alisisitiza kuwa, hivi sasa mitaa ya makazi iko mstari wa mbele zaidi wa mapambano hayo. Takwimu zinaonesha kuwa, hivi sasa wafanyakazi karibu milioni nne wa mitaa ya makazi wanafanya juhudi kubwa ili kulinda mitaa laki 6.5 nchini China. Kazi zao ni pamoja na kupima joto la wakazi, kuwanunulia wakazi chakula na mahitaji mengine ya maisha, na kuwatoa wakati huduma za afya ya kisaikolojia. Wakati huohuo, wakazi wa kawaida wamefuata maagizo ya serikali, na kukaa nyumbani bila ya kutoka mara kwa mara, ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa.
Hadi tarehe 11 mwezi huu, watu wasiopungua 70 wamejitolea kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya korona. Watu hao ni pamoja na polisi 20, madaktari 8, na watumishi kadhaa wa ngazi ya shina.
Pia kuna watu wengine wengi wa kawaida wametoa mchango wao kwa ajili ya mapambano dhidi ya maambukizi. Kati yao ni wamiliki wa migahawa wanaopeleka chakula kwa madaktari, wasambazaji wa vifurushi wanaoshikilia kuwa kazini, na madereva wa taksi wanaohudumia madaktari.
China ina imani kuwa kutokana na juhudi za pamoja za wananchi wote, changamoto ya maambukizi itashindwa haraka.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |