Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango ya Tanzania na Benki Standard Chartered tawi la Tanzania imesema, fedha hizo zitatumika kujenga sehemu yenye urefu wa kilomita 550 za reli kati ya Dar es Salaam na Makutupora, katikati ya Tanzania.
Msemaji wa wizara ya Fedha Bw. Ben Mwaipaja amesema, mkopo huo uliosainiwa jana utalipwa katika kipindi cha miaka 20, lakini hakutoa taarifa zaidi juu ya kiwango cha riba.
Utakapokamilika, mtandao huo wa reli utaiunganisha Tanzania na Burundi, Rwanda, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |