Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametoa wito kwa wananchi wake kushirikiana kukabiliana na matatizo ya uchumi ili kufufua uchumi wa Afrika Kusini.
Rais Ramaphosa amesema hayo katika hotuba yake kuhusu hali ya taifa aliyoitoa jana. Amesisitiza mara nyingi umuhimu wa kuendeleza uchumi na kutoa fursa za ajira, na amekubali kuwa, uchumi wa Afrika Kusini unakabiliana na matatizo mengi, ikiwemo ukosefu wa umeme ulioathiri vibaya uchumi wa nchi hiyo.
Rais Romaphosa amesema, katika miaka miwili iliyopita, Afrika Kusini ilitatua matatizo magumu katika mchakato wa maendeleo ya uchumi na mazingira ya kufanya biashara yanaboreshwa. Ameongeza kuwa, uwekezaji kutoka nchi za nje unaongezeka, uchumi unaendelea kwa utulivu, na hali hiyo imewekea msingi thabiti kwa kufufuka kwa uchumi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |