Baraza la Seneti la bunge la Marekani limepitisha muswada unaolenga kumzuia rais Donald Trump wa nchi hiyo kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran.
Baraza hilo lilipitisha mswada huo jana kwa kura 55 za ndiyo na kura 45 za hapana, huku wanachama 8 wa Republican walipiga kura za ndiyo. Muswada huo ulisisitiza kuwa rais Trump hawezi kuchukua hatua za kijeshi bila ya ridhaa ya bunge.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |