• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jaji mkuu wa Rwanda atoa wito wa kuziba mianya kwenye vita dhidi ya ufisadi

  (GMT+08:00) 2020-02-14 19:05:58
  Jaji mkuu wa Rwanda Bw. Faustin Ntezilyayo ametaka hatua madhubuti zichukuliwe ili kuziba mianya katika vita dhidi ya ufisadi katika sekta ya mahakama nchini humo.

  Akizungumza kwenye mkutano wa kupambana na ufisadi mjini Kigali Alhamisi, Jaji Ntezilyayo amesema huduma mbovu hufungua mianya ya rushwa, na ili kukomesha ufisadi ni lazima mianya yote izibwe. Pia amesema kuna haja ya kutathmini, ikiwa hatua zinazochukuliwa za kupambana na ufisadi zinafanikiwa.

  Rwanda imeweka hatua mbali mbali za kupambana na ufisadi katika sekta ya mahakama, ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfumo wa usimamizi wa kesi kwa njia ya kielektroniki, na kuzuia kuahirishwa kwa kesi bila sababu za kutosha.

  Kwa mujibu wa takwimu kuhusu rushwa zilizotolewa mwezi uliopita na Shirika la Transparency International, Rwanda ndio nchi yenye ufisadi kidogo zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki, na ni ya nne kusini mwa Jangwa la Sahara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako