• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa wito wa ushirikiano wa kimataifa dhidi ya COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-02-14 19:18:20

  Mjumbe wa Baraza la Taifa la China ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi amesema virusi havina mipaka, na jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya kazi kwa pamoja kupigana na virusi vipya vya korona (COVID-19).

  Akizungumza na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Ujerumani Bw. Heiko Maas, Bw. Wang amesisitiza kuwa, katika mapambano ya kulinda afya ya umma, uelewa wa pande zote, kuaminiana na kuungwa mkono na jamii ya kimataifa ni muhimu zaidi. Amesema tangu mlipuko wa ugonjwa huo utokee, serikali ya China imechukua hatua za kina na madhubuti zaidi kudhibiti na kuzuia ugonjwa huo, juhudi hizo zimeanza kuzaa matunda kwani virusi vya korona kwa sasa vimedhibitiwa.

  Bw. Wang amesema, hadi Alhamisi, maambukizi mapya nje ya mkoa wa Hubei yamepungua kwa siku 10 mfululizo, kiwango cha tiba kimeendelea kuongezeka, na zaidi ya wagonjwa 6,000 wameruhusiwa kutoka hospitali. Hata hivyo amekiri kwamba janga hilo limesababisha athari kwa uchumi wa China, lakini ni ya muda mfupi, na anaamini kasi ya ukuaji wa uchumi itaongezeka baada ya janga hilo.

  Naye waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Bw. Mass amesema, nchi hiyo inapinga maoni yoyote ya kibaguzi dhidi ya janga hilo, na itaendelea kulichukulia kwa utulivu. Ameongeza kuwa Ujerumani iko tayari kuendelea kutoa msaada kwa China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako