• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirka la ndege la Ethiopia kuendelea na safari za China

    (GMT+08:00) 2020-02-14 19:39:29

    Shirika la ndege la Ethiopia limesisitiza kuwa litaendelea na safari zake za China na kwamba kupiga marufuku safari hizo haiwezi kuwa njia ya kupambana na virusi vya korona.

    Mkurungezi mkuu wa shirika hilo kubwa zaidi barani Afrika Tewolde Gebremariam amesema badala ya kupiga marufuku safari zake linaimarisha ukaguzi kwa kushirikina na serikali ya China.

    Wito wake huo ni sawa na wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteres ambaye tayari amebaini kuwa WHO haijatoa ushauri wowote wa kutosafiri au kufanya biashara.

    Aidha mkuu wa kituo cha kupambana na maradhi barani Afrika John Nkengasong hivi karibuni amesema kwa sasa kitu muhimu zaidi ni kupambana na virusi hivyo lakini sio kupambana na watu.

    Kufikia mwanzoni mwa wiki hii maafisa wa Ethiopia walikuwa wamepima hali ya joto ya abiria 47,167.

    Ni wachache tu wachache wameonyesha dalili za kuwa na hali tofauti lakini hadi sasa pia barani Afrika hakuna yeyote aliyegunduliwa kuwa na virusi vya korona.,

    Shirika la ndege la Ethiopia hufanya safari 35 kila wiki kwenda miji mitano nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako