• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bandari ya Mombasa yaimarisha oparesheni

    (GMT+08:00) 2020-02-14 19:40:49
    Bandari ya Mombasa nchini Kenya inatarajiwa kuongeza zaidi uwezo wake wa kubeba mizigo na uwasilishaji.

    Mamlaka ya Bandari za Kenya (KPA) imesema katika taarifa yake kuwa meli mpya za kubeba mizigo kwenye bandari zinatarajiwa kubeba mizigo ya ukubwa wa futi 20 kwa safari mara moja.

    Kutokana na kuwepo kwa meli hizo mpya sasa kituo cha kubeba mizigo cha kawaida kinatarajia meli 16 jambazo zitabeba takriban mizigo ya tani 353,533.

    Wakati huo huo, uagizaji wa bidhaa nyingi uliongezeka kwa tani 110,800 katika wiki ya kwanza ya Februari.

    Takwimu za utendaji wa kila wiki zilizokusanywa na Idara ya Kawaida ya Mizigo ya KPA zilithibitisha kwamba shehena kubwa ilichukua asilimia 42.07 ya jumla ya tani 263,384 za tani zilizoshughulikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako