• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • :Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 8-February 14)

  (GMT+08:00) 2020-02-14 19:47:01

  China: Rais Xi Jinping awatembelea wagonjwa wa virusi vya Corona

  Rais wa China, Xi Jinping leo amewatembelea wagonjwa wa virusi vya Corona pamoja na maafisa wa afya ambao wanawahudumia wagonjwa hao.

  Xi alionekana amevalia kitambaa cha kufunika uso kwa ajili ya kujikinga na pia alipima afya yake. Huku akiviita virusi vya Corona kama "janga", Xi amesema hatua kali zaidi zitachukuliwa kwa ajili ya kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.

  Rais Xi amemteua Waziri Mkuu Li Keqiang kuongoza kundi la wafanyakazi litakaloshughulikia mripuko wa virusi hivyo na mwezi uliopita Li aliutembelea mji wa Wuhan ambako virusi hivyo vilianzia. Wakati huo huo, timu ya wataalamu wa Shirika la Afya duniani imeelekea Beijing kuchunguza mripuko wa virusi vya Corona.

  Kwa mujibu wa chombo cha habari cha DW, hadi sasa virusi hivyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 900 na wengine zaidi ya 40,000 wameambukizwa.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako