Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuboresha mfumo wa kukinga na kudhibiti majanga makubwa na utaratibu wa usimamizi wa dharura wa afya ya umma.
Rais Xi ametoa maagizo hayo wakati akiongoza mkutano wa 12 wa kamati ya kuimarisha mageuzi ya pande zote uliofanyika leo hapa Beijing.
Akieleza jukumu kubwa la kulinda afya na maisha ya watu, rais Xi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kuna haja ya kuimarisha maeneo yenye udhaifu na kufunga mianya iliyojitokeza wakati wa janga la sasa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |