• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Mashariki yakumbwa zaidi na uvamizi wa nzige katika miongo kadhaa iliyopita

    (GMT+08:00) 2020-02-15 19:32:57

    Nchi kadhaa za Afrika Mashariki zinateswa na uvamizi wa nzige, na Kenya inakabiliwa vibaya zaidi na uvamizi huo katika miongo saba iliyopita. Ikiwa hawatazuiliwa, nzige hao wanaweza kuongezeka mara 500 mnamo Juni.

    Hayo yamesemwa na msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric. Amesema mbali na Kenya, Somalia na Ethiopia pia zinakabiliwa vibaya zaidi na uvamizi wa nzige katika miaka 25 iliyopita, wakati huohuo, Djibouti, Eritrea, Uganda na Tanzania pia zinashambuliwa na makundi ya nzige, haswa nchini Sudani Kusini, nzige wameenea.

    Dujarric amesema, nchi zinazoathiriwa na zenye hatari kubwa zina mahitaji ya haraka ya misaada, ili kudhibiti nzige wasiongezeke sana, lakini hadi sasa ni dola milioni 20 tu za kimarekani zimeahidiwa ikilinganishwa na mahitaji halisi ya dola milioni 76 yaliyotolewa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako