• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Asilimia ya wagonjwa mahututi walioambukizwa virusi vya korona yaendelea kupungua

    (GMT+08:00) 2020-02-16 19:05:36

    Kamati ya afya ya taifa ya China imesema asilimia ya wagonjwa mahututi kati ya wote walioambukizwa virusi ya Korona, imepungua kwa kasi.

    Msemaji wa kamati hiyo Bw. Mi Feng, amesema mjini Wuhan ambako ni kiini cha maambukiziya ugonjwa huo, asilimia hiyo imeanguka kutoka kilele cha asilimia 32.4 ya Januari 28 hadi asilimia 21.6 ya Februari 15. Na katika mikoa mingine ya China, kiwango hicho pia kimepungua kutoka kwa kilele cha asilimia 15.9 ya Januari 27 hadi asilimia 7.2 ya Februari 15.

    Bw. Mi amesema mabadiliko haya yanathibitisha kuwa hatua za sasa za kuzuia na kudhibiti zina ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako