• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya wagonjwa mahututi wa virusi vya korona yazidi kupungua

    (GMT+08:00) 2020-02-17 09:38:20

    Takwimu zilizotolewa na Kamati ya afya ya China zinaonyesha kuwa hadi kufikia tarehe 15 mwezi huu, idadi ya wagonjwa mahututi wa virusi vya korona inazidi kupungua kote nchini.

    Takwimu zinaonyesha kuwa hadi kufikia tarehe 15 idadi ya wagonjwa mahututi kati ya wagonjwa wote wa virusi vya korona mjini Wuhan, imepungua hadi asilimia 21.6 kutoka asilimia 32.4 ya tarehe 28 mwezi uliopita. Idadi hiyo imepungua hadi asilimia 11.1 katika miji mingine mkoani Hubei, na kiwango hicho imepungua hadi asilimia 7.2 katika mikoa mingine nchini China.

    Msemaji wa Kamati ya afya ya China Bw. Mi Feng amesema mabadiliko hayo yameonyesha kuwa matokeo yamepatikana katika kudhibiti mlipuko wa virusi vya korona nchini kote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako