• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China iko makini katika kudhibiti njia za maambukizi ya virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-02-17 09:38:43

    Ofisa wa Kamati ya afya ya China Bw. Zhou Yuhui amesema China iko makini katika kudhibiti njia za maambukizi katika vita dhidi ya virusi vya korona.

    Amesema kazi kuu kwa sasa ni kudhibiti vyanzo vya maambukizi na kuzuia kuenea kwa virusi, ili kuwalinda wananchi hasa kwa wale waliko hatarini zaidi kuambukizwa. Kamati ya afya ya China itaendelea kuweka mpango mpya juu ya kudhibiti vyanzo vya maambukizi ya virusi vya korona, na kuongoza kazi za mitaani katika kuthibitisha wagonjwa, kuchunguza njia za maambukizi, na kuwafuatilia watu waliokuwa karibu na wagonjwa.

    Ameongeza kuwa watu wanaotoka maeneo yenye hali mbaya ya maambukizi wanafuatiliwa kwa karibu. China pia inapambana vikali na biashara ya wanyamapori, na kuimarisha usimamizi wa soko la wanyamapori, ili kudhibiti chanzo cha hatari dhidi ya afya ya umma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako