• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Klopp amhurumia kocha mwenzake, Pep Guardiola na wachezaji wa Manchester City

    (GMT+08:00) 2020-02-17 10:42:45

    Jurgen Klopp amesema anamhurumia kocha mwenzake, Pep Guardiola pamoja na wachezaji wa Manchester City kwa kufungiwa na kutoshiriki michuano ya Uefa Champions League kwa kipindi cha muda wa miaka miwili. Bosi huyo wa Liverpool amemuacha mpinzani wake City kwa jumla ya pointi 25 kwenye msimamo wa Premier League baada ya kuibuka kwa goli 1 – 0 dhidi ya Norwich. Manchester City imepigwa marufuku kushiriki ligi ya mabigwa Ulaya kwa misimu miwili ijayo baada ya kupatikana wamekiuka sheria za Uefa zinazoambatana na masuala ya fedha na leseni. Bodi ya udhibiti wa masuala ya fedha imesema City imevunja sheria kwa kuweka kiwango cha juu zaidi cha fedha katika mapato yake ya ufadhili kwenye mahesabu yake na katika ripoti ya fedha iliyowasilishwa kwa Uefa kati ya 2012 na 2016 ilionesha kwamba hawakupata hasara wala faida", na kuongeza kwamba klabu hiyo haikutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi". Klabu hiyo kutoka Premier League inatarajiwa kubisha hodi kwenye mahakama ya usuluhisi ikionyesha kutoridhishwa na maamuzi yaliyotolewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako