• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mswada kuhusu kuahirishwa kwa mkutano wa bunge la umma la China kujadiliwa

    (GMT+08:00) 2020-02-17 18:11:03

    Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu utajadili mswada kuhusu kuahirisha mkutano wa 3 wa bunge la awamu ya 13 la umma la China.

    Msemaji wa kamati ya kazi za kisheria ya kamati hiyo Bw. Zang Tiewei amesema, kwa mujibu wa mpango uliotolewa mwaka jana, mkutano huo ulipangwa kufanyika tarehe 5 Machi hapa Beijing.

    Ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vipya vya korona vinavyosababisha nimonia (COVID-19) yaliyotokea nchini China, pia kufanya juhudi zote kudhibiti maambukizi hayo, na kutoa kipaumbele kwa usalama na afya ya umma, Kamati hiyo imependekeza kuahirishwa kwa mkutano wa 3 wa Bunge la Umma la China.

    Kwa mujibu wa sheria, uamuzi huo unahitaji kupitishwa kwenye mkutano wa kamati ya kudumu ya bunge la umma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako