• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kwa nini China ina imani ya kushinda COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-02-17 18:13:40

    Hadi kufikia saa 6 usiku wa tarehe 16, maambukizi ya virusi vipya vya korona vya kusababisha nimonia COVID-19 yamepungua kwa siku 13 mfululizo katika sehemu mbalimbali nchini China licha ya mkoa wa Hubei, na wakati huohuo, zaidi ya wagonjwa elfu 10 wamepata nafuu. China ina imani kubwa ya kushinda COVID-19.

    Mjumbe wa taifa la China Bw. Wang Yi ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje ya China hivi karibuni alipohojiwa na wanahabari wa Shirika la Habari la Ufaransa Reuters amesema, China ina uwezo na imani kushinda COVID-19.

    Imani hiyo inatokana na busara na uwezo mkubwa wa kiutawala wa kiongozi wa China. Rais Xi Jinping ameongoza na kupangilia juhudi za kupambana na maambukizi ya virusi, na kuitisha mkutano katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa jadi wa China. China pia imeanzisha tume maalumu ya kukabiliana na COVID-19 iliyo chini ya uongozi wa rais Xi.

    Imani hiyo inatokana na mfumo bora wa kisiasa nchini China. Baada ya kutokea kwa mlipuko wa COVID-19, serikali ya China imekusanya rasilimali zote, na kuchukua hatua kubwa zaidi kwa pande zote ili kukabiliana na maambukizi ya virusi. Kwa mfano imejenga hospitali maalumu ndani ya siku chache katika sehemu mbalimbali, kutuma madaktari wengi katika mkoa wa Hubei unaoathiriwa zaidi, na kuwaagiza watu zaidi ya bilioni moja kukaa nyumbani bila ya kutoka nje ili kuzuia uenezi wa virusi.

    Imani hiyo pia inatokana na uungaji mkono wa jamii ya kimataifa. Baada ya kugundua maambukizi ya virusi vipya, China imeripoti kwa wakati kwa Shirika la Afya Duniani WHO na jamii ya kimataifa, ili kuzuia uenezi wa ugonjwa duniani. Hadi sasa watu waliothibitishwa kuambukizwa na virusi vipya vya korona nje ya China bado hawajafikia asilimia moja ya wagonjwa wote. Juhudi za China za kupambana na COVID-19 zimeungwa mkono wa jamii ya kimataifa. Viongozi wa nchi na mashirika zaidi ya 160 duniani wametuma salamu kwa China, ili kuiunga mkono, na kati yao makumi ya nchi zimetoa misaada halisi kwa China.

    Aidha, imani hii intokana na ufahamu mzuri wa China kuhusu changamoto zinazoikabili. Changamoto ya kwanza ni tishio la maambukizi ya virusi kwa usalama wa umma, ambao pia ni tishio kwa dunia nzima. China itajumuisha uzoefu kwa makini, ili kujiongezea uwezo, pia itaendelea kuimarisha ushirikiano na nchi mbalimbali duniani, ili kukabiliana na changamoto hiyo kwa pamoja. Changamoto ya pili ni athari iliyosababishwa na COVID-19 kwa maendeleo ya uchumi na jamii. China siku zote inazingatia maisha bora ya wananchi, na inatafuta uwiano wa kupambana na maambukizi ya virusi na ukuaji wa uchumi. Inaaminiwa kuwa ugonjwa utaangamizwa, na uchumi utafufuka kwa haraka.、

    Kama Bw. Wang alivyosema, baada ya kushinda COVID-19, Wachina watashikamana zaidi, uchumi wa China utakua vizuri zaidi, na urafiki kati ya China na nchi nyingine utaimarishwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako