• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahudumu 1,200 wa afya kutoka Jeshi la China wawasili Wuhan

    (GMT+08:00) 2020-02-17 19:37:07

    Jumla ya wataalam 1,200 wa afya, ambao ni kundi la pili la wahudumu 2,600 wa afya waliotumwa na jeshi la ulinzi la China, wamewasili mjini Wuhan hii leo ili kusaidia kudhibiti virusi vya korona.

    Kundi hili limepewa jukumu la kutibu wagonjwa katika tawi la Hospitali ya Huduma kwa Mama na Watoto katika eneo la Optoc Valley mjini Wuhan, na wataanza kazi moja kwa moja baada ya ujenzi kukamilika.

    Wiki iliyopita, China imeahidi kupeleka wahudumu wa ziada 2,600 wa afya kutoka jeshi la nchi hiyo ili kusaidia kudhibiti virusi vipya vya korona mjini Wuhan, na kundi la kwanza liliwasili Wuhan Alhamis iliyopita.

    Mpaka sasa, jeshi la China limepelea wahudumu 4,000 wa afya katika awamu tatu kuisaidia Wuhan katika mapambano dhidi ya mlipuko wa virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako