• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China aongoza kikao cha kukabiliana na maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-02-17 21:11:38

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang ameongoza kikao cha kikundi cha uongozi wa kazi za kukabiliana na maambukizi ya COVID-19 cha serikali kuu ya China kilichofanyika leo.

    Kikao hicho kinaona kuwa hali ya maambukizi ya virusi hivyo nchini China inaonesha mwelekeo mzuri. Kitovu cha maambukizi bado ni mji wa Wuhan na mkoa wa Hubei, hali ya maambukizi bado ni ngumu, na kazi za kinga na udhibiti haziwezi kulegea. Wakati huohuo, kikao hicho kimesema kitaratibu kinga na udhibiti wa maambukizi na maendeleo ya uchumi na jamii.

    Kikao hicho pia kimesisitiza kuwa, mji wa Wuhan na mkoa wa Hubei unatakiwa kuendelea kufanya ukaguzi na kuongeza upatikanaji wa vitanda hospitalini. Serikali kuu nayo itaunga mkono zaidi nguvu ya matibabu kwa kufuata mahitaji, huku ikijumuisha wataalamu kutoa tiba kwa wagonjwa wenye hali mbaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako