• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya wataalamu wa China na WHO yaanza uchunguzi wa virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-02-18 09:16:39

    Timu ya pamoja ya wataalamu kutoka China na Shirika la Afya Duniani WHO imeanza uchunguzi kuhusu kuzuia na kudhibiti mlipuko wa virusi vya korona kwenye maeneo yaliyoathiriwa na virusi hivyo.

    Msemaji wa Kamisheni ya afya ya taifa ya China Bw. Mi Feng amesema timu hiyo imepangwa kwenda Beijing na mikoa ya Guangdong na Sichuan kufanya uchunguzi huo.

    Kwenye kongamano lililofanyika Jumapili ambalo lilihudhuriwa na wataalamu wa timu hiyo na wajumbe wa kikundi cha uongozi wa kukabiliana na mlipuko wa virusi vya korona, naibu mkurugenzi wa kamisheni ya afya ya China Li Bin alitoa ripoti kuhusu hatua zinazochukuliwa kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo, na kuahidi kushirikiana na jumuiya ya kimataifa ili kukabiliana na changamoto za mlipuko wa virusi vya korona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako