• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Dawa za malaria zathibitishwa kuwa na ufanisi wa kutibu nimonia ya COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-02-18 09:17:29

  Wataalamu wa China wamethibitisha kuwa dawa ya malaria aina ya Chloroquine Phosphate ina ufanisi wa kutibu ugonjwa wa nimonia unaosababishwa na virusi vya korona COVID-19.

  Naibu mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Maendeleo ya Teknolojia ya Viumbe kilicho chini ya Wizara ya Sayansi na Teknolojia ya China Bibi Sun Yanrong, amesema wataalamu wamependekeza kuiweka dawa hiyo kwenye mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa huo na kufanya majaribio zaidi ya dawa hiyo kwa binadamu haraka iwezekanavyo.

  Dawa ya Chloroquine Phosphate ambayo imetumiwa kwa zaidi ya miaka 70 kutibu ugonjwa wa malaria, imechaguliwa miongoni mwa mamia ya maelfu ya dawa zilizopo baada ya kufanyiwa majaribio.

  Kwa mujibu wa ofisa huyo, dawa imeanza kufanyiwa majaribio kwa wagonjwa katika hospitali zaidi ya kumi mjini Beijing na katika mikoa ya Guangdong na Hunan, na imeonesha ufanisi dhidi ya virusi vya korona. Amesema wagonjwa zaidi ya mia moja waliotumia dawa hiyo wamepona haraka zaidi na mpaka sasa hakuna madhara au athari hasi zilizoripotiwa kutokana na matumizi ya dawa hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako