• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Adui mkubwa zaidi sio virusi vya korona, bali ni habari za kupotosha zinazoweza kuwatenga watu

  (GMT+08:00) 2020-02-18 18:36:03

  China bado inajitahidi kupambana na maambukizi ya virusi vipya vya korona vinavyosababisha nimonia (COVID-19). Wakati huohuo, badala ya kutoa misaada, baadhi ya nchi za magharibi zinapaka matope China kutokana na ugonjwa huo. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri inayouliza, "Adui mkubwa zaidi kuliko virusi ni nini".

  Tangu mlipuko wa mambukizi ya virusi vipya vya korona vinavyosababisha nimoni (COVID-19) utokee, serikali ya China imeongoza wananchi bilioni 1.4 kukabiliana na virusi hivyo kwa nia na ujasiri mkubwa. Hospitali mbili kubwa zilijengwa mjini Wuhan ndani ya siku zaidi ya kumi, maelfu ya madaktari wamejitolea kutoa msaada wa matibabu mkoani Hubei, na zaidi ya Wachina bilioni moja wamekaa nyumbani bila ya kutoka nje ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi.

  Wakati huohuo, baadhi ya nchi za magharibi zinailaumu China, zikisema haichukui hatua madhubuti na inaficha habari, ili kupaka matope mfumo wa kisiasa wa China. Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Biashara ya Marekani Peter Navarro amesema China ni "kitotoa cha virusi", kauli iliyokosolewa na mke wa waziri mkuu wa Singapore, akiuliza kwenye mtandao wa kijamii kuwa, kama ni hivyo, maambukizi makubwa ya mafua yanayotokea nchini Marekani yamefichua nini? Waziri wa Biashara wa Marekani Wilbur Ross alisema maambukiziya virusi vya korona nchini China yataziharakisha kampuni za uzalishji kurudi nchini Marekani. Vyombo vya habari vya Marekani viliporipoti hospitali zilizojengwa mjini Wuhan, havikuzumzia jinsi hospitali hizo zitakavyosaidia katika kukabiliana na maambukizi ya virusi, bali vilisema hospitali hizo zitakuwa hasara baada ya kushinda ugonjwa.

  Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Ghebreyesus ameipongeza China kwa kuchukua hatua mwafaka ili kuzuia maambukizi ya COVID-19, na kujitoa mhanga ili jumuiya ya kimataifa ijiandae zaidi. Lakini jambo linaloshangaza ni kwamba, kuna wanahabari wa nchi za magharibi wenye mashaka kuwa Mkurugenzi huyo amesema hayo kwa kulazimishwa na serikali ya China. Kama Bw. Ghebreyesus alivyosema, wakati wa kukabiliana na virusi, jamii ya kimataifa pia inapaswa kupambana na habari za kupotosha. Adui mkubwa zaidi si virusi, bali ni vitendo vya kupaka matope vinavyoweza kutenganisha watu.

  Hivi sasa badala ya kuwa na hofu kubwa, jambo tunalopaswa kufanya ni kupambana na virusi. Badala ya kukaa kimya, nchi mbalimbali duniani zinapaswa kujitahidi kwa pamoja, kwani katika wakati huu muhimu, tunachohitaji zaidi ni mshikamano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako