• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaitaka Marekani kuacha vitendo vya uchochezi

  (GMT+08:00) 2020-02-18 18:45:46

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inahimiza Marekani kushughulikia kwa haki kampuni za China na ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili na kuacha vitendo vya uchochezi.

  Kuhusu Marekani kutaka kutoa muswada kuzuia kampuni ya GE ya nchi hiyo kutoa injini kwa ndege ya aina ya C919 ya China kutokana na hofu ya China kuiga mchakato wa utengenezaji, Bw. Geng amesema, kampuni hiyo imesema, kuiga utengenezaji wa injini ni vigumu zaidi kuliko inavyofikiriwa na maofisa wa Marekani. Amesema kampuni hiyo imeanzisha ushirikiano na China kwa miaka nyingi, na kama China ilitaka kuiga, isingesubiri mpaka sasa.

  Bw. Geng amesema, kitendo hicho kimeonesha baadhi ya maofisa wa Marekani hawana uzoefu wa kisayansi, wanapuuza kanuni ya soko na kuhofu maendeleo ya China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako