• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema waraka wa China ni muhimu katika kuwezesha Shirika hilo kutoa ushauri

    (GMT+08:00) 2020-02-18 19:01:30

    Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa waraka wa hivi karibuni wa China kuhusu COVID-19 ni muhimu katika kuliwezesha kutoa ushauri kwa nchi nyingine.

    Mkurugenzi mkuu wa WHO, Tedros Ghebreyesus amesema, waraka huo uliotolewa jana na China, unaoeleza kwa uwazi kuhusu zaidi ya kesi elfu 44 zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya COVID-19, unatoa uelewa mzuri kuhusu umri wa watu walioathirika, ukali wa ugonjwa na kiwango cha vifo.

    Amesema taarifa hizo ni muhimu katika kuiwezesha WHO kutoa ushauri mzuri wenye ushahidi kwa nchi nyingine, na kuzitaka nchi zote kubadilishana taarifa zao kwa uwazi.

    Bw. Ghebreyesus amesema, hivi sasa timu ya wataalam wa kimataifa wa WHO iko nchini China ikishirikiana na wenzao wa China ili kuelewa vizuri na kuboresha uelewa wa mlipuko wa virusi vya korona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako