• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China azungumza na viongozi wa Uingereza na Ufaransa kuhusu COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-02-18 20:55:54

    Rais Xi Jinping wa China leo kwa nyakati tofauti amezungumzo kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa.

    Katika mazungumzo hayo, rais Xi amesema China imefanikiwa kudhibiti maambukizi ya virusi vipya ya korona vinavyosababisha nimonia duniani, na inapenda kushirikiana na jamii ya kimataifa kupambana na ugonjwa huo.

    Alipozungumza na Bw. Boris, rais Xi amesema, China imefanya juhudi kubwa, na kupata ufanisi katika kudhibiti kuenea kwa COVID-19 duniani, na itaendelea kushirikiana na nchi mbalimbali duniani ikiwemo Uingereza. Ameongeza kuwa zikiwa nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China na Uingereza zinapaswa kushirikiana na kubeba jukumu kubwa zaidi ili kukabiliana na changamoto zinazoongezeka duniani.

    Kwa upande wake, Bw. Boris ameipongeza China kwa kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na maambukizi ya virusi, na kutoa taarifa kuhusu virusi kwa wakati, amesema Uingereza itaendelea kutoa misaada na kuiunga mkono kwa China.

    Katika mazungumzo yake na rais Macron, Rais Xi amesema, China itaendelea kufuata msimamo wazi, na kushirikiana na jamii ya kimataifa ikiwemo Ufaransa katika mapambano dhidi ya COVID-19.

    Naye Rais Macron amesema Ufaransa inapenda kupambana na COVID-19 pamoja na China, na kuongeza ushirikiano na China katika sekta ya afya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako