• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalam wasisitiza kutumia dawa ya jadi ya kichina katika kupambana na virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-02-19 09:20:58

    Mtaalamu wa magonjwa kwenye mfumo wa kupumua Bw. Zhong Nanshan amesisitiza utafiti wa dawa ya jadi ya kichina TCM kwenye mapambano dhidi ya nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vya korona.

    Akizungumza kwenye mkutano na wanahabnari uliofanyika jana mjini Guangzhou, Bw. Zhong amesema dawa ya mitishamba iitwayo Nimonia No. 1 iliyotolewa Januari 23 imethibitishwa kuwa na ufanisi katika kutibu wagonjwa wa COVID-19 mkoani Guangdong.

    Kwa mujibu wa mtaalam huyo, watafiti wanazifanyia majaribio dawa za jadi za kichina zilizopo, ili kujua kama zinaweza kuviangamiza virusi vya korona, kuzuia uvamizi wa virusi hivyo dhidi ya chembechembe za mwili na kupunguza makali ya madhara ya virusi hivyo kwa mfumo wa kinga yaitwayo Cytokine Storm, ambayo husababisha vifo vya wagonjwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako