• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza kilimo cha majira ya mchipuko na mazingira tulivu ya ajira

    (GMT+08:00) 2020-02-19 09:21:25

    Baraza la serikali la China jana Jumanne lilisisitiza umuhimu wa kuanza kilimo kwa wakati kwenye majira ya machipuko na uwepo wa mazingira tulivu ya ajira.

    Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wa baraza hilo ulioongozwa na waziri mkuu Bw. Li Keqiang, inaziagiza serikali za mitaa kutekeleza majukumu ya kuongoza shughuli za kilimo kwenye msimu wa mchipuko ili kuhakikisha uzalishaji tulivu wa kilimo na mavuno.

    Taarifa inasema juhudi zinatakiwa kufanywa kuhimiza mashirika ya kilimo yanayojishughulisha na mbegu, mbolea, dawa za kuulia wadudu na uzalishaji wa chakula cha mifugo, kurejesha uzalishaji, na kuhakikisha ugavi na njia za kusafirisha vifaa na pembejeo za kilimo.

    Mkutano huo pia umeamua kusamehe kwa muda malipo ya bima ya kijamii ili kupunguza athari ya mlipuko wa virusi vya korona na kuhakikisha mazingira tulivu ya ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako