• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afrika ina mengi ya kujifunza kutokana na juhudi za China kupambana na mlipuko wa virusi vya korona

  (GMT+08:00) 2020-02-19 17:02:41

  Mlipuko wa virusi vya Korona kwa sasa ni suala ambalo linaendelea kugonga vichwa vya habari kote duniani. Athari za janga hili zimedhihirika pakubwa nchini China. Kwa sasa, idadi kubwa ya miji yamewekwa karantini.

  Kupambana dhidi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi hivi, ambayo kwa sasa inatambulika rasmi kwa jina COVID-19, bila shaka ni jambo ambalo limepewa kipaumbele na serikali ya China na taifa zima.

  Tangu kutangazwa kwa mlipuko huo, China imefanya kila juhudi kupambana na ugonjwa huo. Kiwango na kasi ya juhudi hizi kutoka taifa hilo haijawahi kushuhudiwa. Ni mapema mno kusema ni lini ushindi utatangazwa, lakini hadi sasa, inaonekana hatua zilizochukuliwa na China zimesaidia pakubwa kuzuia mamilioni ya watu kuambukizwa ugonjwa huo. Baadhi ya wachunguzi wanahoji kuwa labda hali ingekuwa mbaya zaidi iwapo China haingechukua hatua za haraka au iwapo taifa hilo halingekuwa na uwezo wa kukabiliana na janga hili.

  Baada ya thibitisho la mlipuko huo, China iliweka hatua madhubuti ambazo kwa kweli zimehakikisha kwamba idadi ya wale walio na maambukizi ni ndogo mno. Hatua hizi zinastahili kuigwa na mataifa ulimwenguni hasa katika bara la Afrika.

  Hatua ya kwanza iliyochukuliwa na China ni kuanzishwa kwa kituo cha pamoja iliyopewa jukumu la kuratibu hatua zitakazochukuliwa ili kupambana na mlipuko wa virusi hivyo.

  Tangu mwanzo, serikali kuu ya China iliweka bayana kwamba maisha ya raia wake yalistahili kupewa kipaumbele. Ili kufikia hili, serikali kwa haraka ilianzisha jopo kazi ambalo jukumu lake kuu ni kuhakikisha kwamba masuala yote ya dharura yameshughulikiwa mara moja.

  Lakini kazi kubwa zaidi labda ilikuwa ni jinsi gani nchi hiyo ingehamasisha taifa zima la China ili kila raia atekeleze wajibu muhimu katika vita hivi. Kwa mujibu wa sharia, mikoa yote 31 nchini China yalichukua hatua za kina na za dharura ili kukinga umma kutokana na maradhi hayo kwa upesi. Na baadaye ilikuwa bayana kwamba wananchi wote walikuwa tayari kuwa sehemu ya juhudi hizo.

  Maelfu ya wataalamu, vikosi vya matibabu, wahandisi, wafanyakazi wa ujenzi na wengine wengi zaidi walipelekwa katika maeneo yaliyoathirika na mlipuko huo zaidi kama vile mji wa Wuhan.

  Jamii zote katika maeneo ya mijini na mashambani yaliongoza juhudi za kudhibiti usafi. Hali kadhalika, raia wamekuwa wakitoa ripoti kuhusu hali ilivyo walipo kila siku, ili kupunguza maambukizi ya virusi.

  Aidha, mlipuko huo ulizuka wakati Wachina walikuwa wakisubiri sikukuu ya spring, ambao ni mwaka mpya kwa kalenda ya kilimo ya China, na ni sikukuu muhimu zaidi katika jamii ya Wachina. Huu ni msimu ambao familia na marafiki, wanakutana au kutembeleana. Lakini, tangu janga hilo, watu wote wamejikuta nyumbani kwa ajili ya kutii amri ya karantini.

  Lakini labda ishara kubwa ya umoja kwenye vita hivi imedhihirika pale taifa zima imesonga mbele kwa pamoja. Katika kitovu cha mlipuko huo, yaani mkoa wa Hubei na hasa Wuhan, ambao ni mji mkuu wa mkoa huo, wenyeji hawakupigana na ugonjwa huo peke yao. Zaidi ya wafanyakazi wa matabibu 23,000 wamefikishwa mkoani humo ili kutoa msaada wowote unaohitajika.

  Hospitali maalumu mbili mpya yenye uwezo wa kubeba vitanda 2600 yalijengwa kwa haraka ili kutoa matibabu kwa wale walioambukizwa virusi hivyo mjini Wuhan. La kushangaza ni kwamba, hospitali hizo zilijengwa kwa muda wa historia ya chini ya siku 10. Kliniki kadhaa pia zimeanzishwa kuwatibu wagonjwa wenye hali sisizo mbaya sana.

  Wakati huo huo, kituo cha China cha kudhibiti magonjwa CDC na baadhi ya wanasayansi mashuhuri kutoka China pamoja na wenzao kutoka shirika la afya duniani WHO wanaendeleza juhudi za pamoja za kuandaa chanjo na tiba za virusi hivyo.

  Ama kwa kweli, hatua za kuzuia na kudhibiti maradhi hayo yameimarishwa. Wagonjwa wanachunguzwa, taarifa zao kutolewa, wanatengwa na kisha kutibiwa pasipo kupoteza muda. Wale ambao wamekuwa karibu na wale waliopatikana na virusi hivyo pia wanafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

  Jitihada hizi zote zina lengo la kuzuia kuenea zaidi kwa virusi hivyo.

  Katika kipindi hiki, itakumbukwa kuwa China imetekeleza shughuli hizi zote kwa uwazi. Serikali ya China imekuwa ikitoa habari kila wakati kuhusu hali ilivyo nchini humo kila siku.

  Mabalozi ya China nje ya nchi pia zimeendelea kufuatilia kuingia kwa raia wa China katika nchi nyingine. Raia wote kutoka China wametakiwa kujitenga wenyewe nyumbani kwa siku 14 hata kama hawana dalili za virusi hivyo mradi tu wamesafiri kutoka nchi hiyo.

  Kwa raia wa kigeni waonaofanya kazi au kusoma nchini China, serikali ya nchi hiyo imekuwa ikijaribu kutoa huduma nzuri za matibabu na bidhaa za matumizi ya kila siku kwao ili kuwaondolea mzigo wa kuzihangaikia.

  Vyombo vya habari nchini humo pia vimetekeleza wajibu muhimu katika vita hivi. Vyombo hivyo vimekuwa vikitoa habari muhimu kuhusu njia za kuzuia kuenea zaidi kwa virusi hivyo vya korona.

  Juhudi hizi zimepongezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye anasema hatua za China ni za kuvutia sana.

  Mlipuko huu ni dharura ya afya duniani ambayo kuna uwezekano kuwa nchi maskini hayangeweza kukabiliana nayo. Afrika, kwa mfano, bado huathirika na mifumo ya afya dhaifu.

  Juhudi za nchi za Afrika Magharibi katika kupambana na mlipuko wa Ebola kati ya 2014 na 2016 na hivi karibuni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni ushuhuda tosha. Ukweli ni kwamba mataifa hayo yalishindwa kudhibiti ugonjwa huo.

  Hii ndio sababu China inastahili kuigwa na wote kwa jinsi ambavyo imepambana na mkurupuko wa COVID-19. China kwa sasa ni mshirika mkuu wa kibiashara wa Afrika na inatarajiwa kuwa viongozi kutoka bara hilo wanajifunza kutoka kwa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi wa pili duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako