• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kushinda COVID-19 kwa niaba ya jumuiya yenye hatma ya pamoja

  (GMT+08:00) 2020-02-19 17:26:05

  Tangu kutokea kwa maambukizi ya virusi vipya ya korona vinavyosababisha nimonia (COVID-19), watu wa nchi mbalimbali duniani wameeleza kuiunga mkono China.

  Rais Moon Jae-in wa Korea ya Kusini amesema, nchi yake na China ni majirani, kusaidia jirani ni sawa na kujisaidia mwenyewe. Msichana mmoja wa Japan alitembea kwenye mitaa ya Japan akiomba msaada kwa ajili ya China. Wakazi wengi wa mji wa Jerusalem walikwenda Ukuta wa Kulia kuomba baraka kwa China, na mwanamuziki wa Ubelgiji alitunga wimbo kwa ajili ya mji wa Wuhan.

  Aidha, mabalozi wa nchi kadhaa nchini China wametoa video za kutakia China baraka na heri. Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki amesema, Watanzania wako pamoja na China, na kuamini kuwa China itashinda virusi. Pia ameishukuru China kwa kuwasaidia wanafunzi wa Tanzania waliokwama mjini Wuhan. Naye Balozi wa Rwanda nchini China Bw. James Kimonyo amesema, Rwanda inaamini serikali na watu wa China watashinda vita dhidi ya COVID-19.

  Nchi tofauti ziko katika dunia moja. Katika miaka ya hivi karibuni, wazo la jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja lililotolewa na rais Xi Jinping wa China limepokelewa na nchi nyingi, na limewekwa kwenye maazimio husika ya Umoja wa Mataifa. Wakati China inapopambana na maambukizi ya COVID-19, jamii ya kimataifa imeiunga mkono na kutoa misaada ya aina mbalimbali, na hali hii pia imeonesha wazo hilo.

  Katika zama ya utandawazi, changamoto inayokabili nchi moja inaweza kuenea duniani kote, na kutishia jamii ya kimataifa. Ingawa maambukizi ya COVID-19 yametokea nchini China, lakini binadamu wote wanaathiriwa. China imechukua hatua kali na za pande zote ili kukabiliana na maambukizi hayo, ili kuzuia yasienee katika sehemu nyingine duniani, kwani China inajua hili ni jukumu la kimataifa inayopaswa kubeba.

  Rais Xi amesema, kwa kufuata wazo la jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, China si kama tu inawajibika na usalama na afya ya wananchi wake, bali pia inawajibika na shughuli za afya duniani. China itaendelea na msimamo wa wazi, na kushirikiana na nchi mbalimbali duniani. Kutokana na uungaji mkono na misaada ya dunia, China hakika itashinda vita hiyo dhidi ya COVID-19.

  Jamii ya kimataifa inapaswa kushirikiana vizuri ili kuishinda changamoto hii kubwa. Ikiwa dunia ni nzuri, China itakuwa nzuri, na China ikiwa nzuri, dunia itakuwa nzuri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako