• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chombo cha anga ya juu cha Chang'e-4 chaanza kazi tena siku ya 15 ya mwandamo wa mwezi

    (GMT+08:00) 2020-02-19 18:10:06

    Chombo cha anga ya juu cha China kinachoitwa Chang'e kimeanza tena kazi yake ya uchunguzi kwa siku ya 15 ya mwandamo baada ya kulala wakati wa usiku wa baridi kali.

    Sehemu ya kutua ya chombo hicho iliamka saa 12:57 asubuhi Jumanne, na sehemu ya kuzunguka iliamka saa 11:55 jioni Jumatatu.

    Habari zilizotolewa na Kituo cha uchunguzi wa mwezini na angani cha taifa la China, sehemu hizo zote mbili ziko katika hali nzuri ya utendaji kazi.

    Sehemu ya kuzunguka iitwayo Yutu-2 imesafiri mita 367.25 upande wa mbali wa mwezi, ikiwa na mpango wa kwenda kaskazini magharibi kisha kusini magharibi kuendelea na uchunguzi wa kisayansi.

    Chombo cha Chang'e -4 kilichozinduliwa tarehe 8 Desemba mwaka 2018 kilitua sehemu ya Von Karman Crater katika bonde la kusini la Aitken upande wa mbali wa mwezi tarehe 3 Januari mwaka 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako