• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • WHO yasema China inajitihadi kutibu wagonjwa wa COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-02-19 18:13:49

  Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Mipango ya Dharura iliyo chini ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Bw. Michael J. Ryan amesema, idara za afya ya China zinajitahidi kutibu wagonjwa wa nimonia iliyosababishwa na virusi vipya ya korona COVID-19, kupunguza kiwango cha vifo na kuchukua hatua kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

  Bw. Ryan pia amesema, uzoefu uliopatikana na mkoa wa Hubei China wa kupambana na ugonjwa huo umetumiwa katika sehemu mbalimbali, na mfumo wa kisasa wa afya wa China umewawezesha wagonjwa mahututi kupata matibabu yanayofaa mapema.

  WHO pia imesema, China imechukua hatua nzuri ya afya ya umma kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo ambayo imeipa dunia muda wa kujiandaa kupambana na ugonjwa huo.

  WHO inatoa wito kwa nchi mbalimbali kuharakisha uchunguzi wa ugonjwa huo na kubadilishana zaidi habari kuhusu ugonjwa huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako