• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Libya yasitisha kwa muda mazungumzo ya amani baada ya bandari ya Tripoli kushambuliwa

  (GMT+08:00) 2020-02-19 18:16:35

  Serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa imesitisha kwa muda mazungumzo ya amani yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa baada ya jeshi la mashariki mwa nchi hiyo kushambulia bandari ya Tripoli kwa mizinga iliyoanguka karibu na tenki la gesi.

  Umoja wa Mataifa umekuwa unaandaa mazungumzo ya amani mjini Geneva ili kusimamisha vita kati ya serikali ya Libya na jeshi la mashariki la LNA ambalo limekuwa likijaribu kudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo kwa karibu mwaka mmoja uliopita na kusababisha watu wasiopungua laki 1.5 kukimbia maskani yao.

  Serikali ya Libya imetoa taarifa ikisema itasimamisha mazungumzo ya amani hadi hatua thabiti zitakapochukuliwa dhidi ya washambuliaji, na itachukua hatua hizo kwenye wakati mwafaka.

  Serikali hiyo pia imesema mazungumzo hayana maana yoyote bila ya msingi wa kusimamisha kabisa vita, kurudisha watu waliokimbia makazi yao na kuhakikisha usalama wa mji mkuu na miji mingine.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako