• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yajitahidi kutibu wagonjwa wa COVID-19 wakati idadi ya vitanda vya hospitali katika kiini cha mlipuko inazidi elfu 40

  (GMT+08:00) 2020-02-20 09:10:28

  China inafanya juhudi zote kuwatibu wagonjwa wa nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vya korona katika mji wa Wuhan ambao ndio kiini cha mlipuko wa virusi hivyo, wakati idadi ya vitanda vya hospitali kwa ajili ya wagonjwa wa COVID-19 imeongezeka na kuzidi elfu 40, huku idadi ya wafanyakazi wa afya waliojitolea kutoka nje ya mkoa, ikizidi elfu 30.

  Naibu waziri mkuu wa China Bibi Sun Chunlan ambaye ni kiongozi wa timu ya serikali kuu ya kuelekeza kazi ya udhibiti wa mlipuko wa virusi vya korona, aliwatembelea wafanyakazi wa afya walioko katika mstari wa mbele mjini Wuhan na kutaka wagonjwa watibiwe kwa juhudi zote.

  Bibi Sun amesema ni muhimu kujumuisha uzoefu kwa wakati na kuweka itifaki za matibabu ambazo zinaweza kuenezwa.

  Afisa huyo pia ametoa wito wa juhudi za pamoja kufanywa kuwatibu wagonjwa mahututi ili kupunguza kiwango cha vifo kutokana na virusi vya korona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako