• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hali ya udhibiti wa nimonia ya COVID-19 mkoani Hubei yaboreka

  (GMT+08:00) 2020-02-20 09:32:35

  Hali ya udhibiti wa maambukizi ya nimonia ya COVID-19 katika mkoa wa Hubei ambao ni kiini cha mlipuko wa virusi vya korona nchini China, inaendelea kuboreka.

  Msemaji wa Kamisheni ya Afya ya Taifa ya China Bw. Mi Feng amesema hayo kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika jana mjini Beijing, akichambua data za maambukizi ya virusi vya korona mkoani Hubei katika wiki iliyopita.

  Amesema idadi ya wagonjwa waliopona na kuruhusiwa kuondoka hospitali kwa siku mkoani Hubei, mbali na mji mkuu wake Wuhan, imezidi ile ya wagonjwa wapya kwa siku nne mfululizo mpaka jana.

  Afisa huyo pia amesema idadi ya wagonjwa wapya wanaothibitishwa kila siku mkoani Hubei imepungua kwa kiasi kikubwa tangu Februari 13, hali ambayo imeonesha kuwa hali ya mlipuko wa virusi vya korona na kiwango cha uponaji mkoani Hubei vimeboreka kutokana na hatua madhubuti za udhibiti zinazochukuliwa, na kuimarishwa kwa uungaji mkono wa kimatibabu kutoka nje ya mkoa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako