• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kupambana na biashara ya dawa za kulevya kwenye bandari binafsi

    (GMT+08:00) 2020-02-20 09:46:39

    Waziri wa usalama wa Kenya Bw. Fred Matiang'i amesema serikali ya Kenya itachunguza, kusimamia na kuandikisha upya bandari binafsi na vituo binafsi takriban 700 vya kupakua mizigo nchini kote, ili kupambana na biashara ya kimataifa ya dawa za kulevya pamoja na magendo ya bidhaa zilizopigwa marufuku.

    Bw. Matiang'i amesema amezungumza na waziri wa usafiri wa Kenya Bw. James Macharia kuhusu kusimamia na kuandikisha upya bandari zote na vituo vyote vya kupakulia mizigo hasa katika sehemu ya pwani ya Bahari ya Hindi. Amesema vituo vingi haviko chini ya usimamizi wa serikali, hali ambayo imesababisha kuongezeka kwa vitendo haramu vya makundi ya biashara ya kimataifa.

    Bw. Matiang'i ameongeza kuwa kazi ya kuandikisha upya bandari itaanza rasmi mwezi Julai, ili kuhakikisha usalama wa taifa na wananchi, na kuunga mkono biashara halali na uchumi wa Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako