• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa msaada wa vifaa vya kupima virusi vipya vya korona kwa Japan

    (GMT+08:00) 2020-02-20 18:19:41

    China imetoa msaada wa vifaa vya kupima virusi vipya vya korona COVID-19 kwa Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Kuambukiza ya Japan.

    Baada ya idara husika kutenga mamia ya watalii waliokuwa kwenye meli ya Diamond Princess, Japan ilikabiliwa na ukosefu wa vifaa vya kupima virusi vipya vya korona. Muda rasmi wa kuwatenga watu waliokuwa kwenye meli hiyo ulimalizika jana, na watu 621 waliokuwa ndani ya meli hiyo wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo.

    Ubalozi wa China nchini Japan umesema, virusi havina mpaka, China iko tayari kutoa msaada kwa Japan kadri iwezavyo, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano, na kushirikiana kwa pamoja ili kushinda mapambano dhidi ya virusi hivyo mapema zaidi, na kulinda afya na usalama wa watu wa pande zote mbili, wa kikanda na duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako