• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Kigali kuwa mwenyeji wa mkutano wa wakulima na wasindikaji kahawa duniani

    (GMT+08:00) 2020-02-20 19:58:37

    Wakulima wa kahawa na wasindikaji kutoka sehemu mbalimbali duniani watakutana nchini Rwanda mwaka 2021 ili kutathmini changamoto zilizopo katika mnyororo wa thamani wa kahawa.

    Kigali itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa tatu wa wazalishaji kahawa duniani ,ambao utawaleta pamoja watu 1,500 kutoka zaidi ya nchi 40 zinazozalisha kahawa duniani.

    Mkutano huo ambao utafanyika mwezi Julai,pia utavutia viongozi katika sekta hiyo,wanauchumi na wachambuzi haswa kutafuta ufumbuzi wa changamoto ambazo wazalishaji kahawa wanakutana nazo.

    Tangu kuanzishwa kwa mkutano huo 2017 unaoandaliwa mara mbili kwa mwaka,umekuwa ukifanyika nchini Colombia na Brazil.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako