• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar-Wadau sekta ya utalii watakiwa kutafuta ufumbuzi wa changamoto katika uendeshaji wa sekta hiyo

    (GMT+08:00) 2020-02-20 19:59:46

    Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya kale Zanzibar ,Mh.Mahmoud Thabit Kombo amewataka wadau wa sekta ya utalii kuweka wazi hatua za kutatua kasoro za uendeshaji wa sekta hiyo Zanzibar zilizochukuliwa kwa pamoja na serikali.

    Akizungumza katika kikao kati ya wadau wa sekta ya utalii na viongozi wa Jumuiya ya kuratibu masuala ya utalii nchini Italia ,amesema hatua hiyo itawezesha kupunguza malalamiko kutoka kwa wawekezaji wa sekta hiyo inayochangia pato kubw ala taifa.

    Waziri Mahmoud amefahamisha kuwa miongoni mwa juhudi hizo ni pamoja na kuimarisha huduma na ujenzi uwanja wa ndege ,na barabara mbalimbali na pamoja na kuanzishwa mfumo wa kisasa wa kupata viza kwa wageni kwa njia ya kielektroniki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako