• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yawarejesha nchini mwao raia 76 wa Ethiopia waliokuwa Kenya

    (GMT+08:00) 2020-02-20 20:08:08

    Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema limewasaidia wakimbizi 76 wa Ethiopia waliokuwa wanaishi kwenye kambi mbili za wakimbizi kaskazini mwa Kenya kurejea makwao.

    Mwakilishi wa UNHCR nchini Kenya Fathiaa Abdalla amesema, hii ni moja ya sababu kuu za uamuzi wa Shirika hilo kuwa, mpango wa kurejesha wakimbizi lazima uwe wa hiari na wa hatua kwa hatua, ili kuhakikisha kuwa unadumu.

    Hii ni awamu ya kwanza ya wakimbizi kuondoka kwa hiari katika mpango wa kurejesha kundi kubwa la wakimbizi wa Ethiopia waliokuwa katika kambi za Kakuma na Dadaab kaskazini mwa Kenya.

    Jumla ya wakimbizi 28,560 wa Ethiopia wanaishi katika kambi za wakimbizi nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako