• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaongeza kasi ya kugundua chanjo dhidi ya virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-02-21 17:41:35

    Wanasayansi nchini China wanajitahidi kugundua chanjo dhidi ya virusi vya korona COVID-19 kwa kutumia mitazamo mitano ya teknolojia.

    Makamu mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Afya nchini China Zeng Yixin amesema, mitazamo hiyo ni pamoja na kutumia chanjo ambazo hazijatumika, na chanjo kwa kutumia dawa zinazotibu mafua. Amesema kuanzia mwezi Aprili mpaka Mei mwaka huu, baadhi ya chanjo zinaweza kuanza kutumika kwa majaribio, ama chini ya mazingira maalum, zitaweza kutumika kwa dharura tu.

    Wakati huohuo, mji wa Wuhan ulioathiriwa zaidi na mlipuko wa virusi vya korona umeonyesha kuwa, kwa mara ya kwanza, idadi ya watu waliopona ugonjwa huo na kuruhusiwa kutoka hospitali imezidi ile ya kesi za maambukizi mapya zilizothibitishwa.

    Msemaji wa Tume ya Taifa ya Afya nchini China Mi Feng amesema, idadi mpya ya watu walioruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupona kwa siku moja imepita elfu 2 kwa mara ya kwanza hapo jana. Ameongeza kuwa, kiwango cha watu waliopona mjini Wuhan, mji mkuu wa mkoa wa Hubei, na katika maeneo mengine ya mkoa huo imeendelea kuongezeka katika wiki iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako