• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Urafiki wa kindugu kati ya China na Afrika waimarishwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-02-21 17:43:40

  Tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vipya vya korona COVID-19 nchini China, Afrika haikusita kutoa misaada na uungaji mkono. Urafiki wa kindugu kati ya China na Afrika umekuwa ukiimarishwa katika ushirikiano wa kukabiliana na ugonjwa huo, na jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika itazidi kuwa imara.

  Tangu kutokea kwa ugonjwa huo mjini Wuhan, China, China imepokea misaada kutoka nchi na sehemu mbalimbali duniani, kati ya misaada hiyo, ile ya kutoka baadhi ya nchi za Afrika inathaminiwa zaidi. Comoros, iliyoko upande wa magharibi wa bahari ya Hindi, ni moja kati ya nchi maskini zaidi. Ingawa EURO 100 zilizochangwa na Shirikisho la urafiki kati ya Comoros na China si fedha nyingi, lakini urafiki unaooneshwa kupitia mchango huo ni mkubwa.

  Mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika umemalizika hivi karibuni. Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo wametangaza kwa pamoja kuwa, katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID-19, Afrika inasimama bega kwa bega na serikali na watu wa China. Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa ya Kuambukiza kimetoa wito wa kutoiwekea China vizuizi vya kufanya biashara,utalii na mawasiliano ya kuvuka mipaka. Shirika la ndege la Ethiopia ambalo ni shirika kubwa zaidi la ndege barani Afrika, lilitangaza kuwa litaendelea na safari zake nchini China.

  Msimamo wa kuwajibika wa China unaooneshwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo umetoa picha kubwa kwa nchi mbalimbali barani Afrika. Naibu mwenyekiti wa chama cha Conservative wa Misri Bw. Mohammed Amin anasema:

  "Ili kupambana na ugonjwa huo, China imejenga hospitali maalumu mjini Wuhan ndani ya muda mfupi. Tunaipongeza China kwa hatua zake za kukabiliana na ugonjwa huo. Nataka kusema: Endelea Wuhan! Endelea Chinaļ¼"

  Tokea mlipuko wa ugonjwa huo utokee, serikali ya China imefuata msimamo wa wazi kufanya ushirikiano wa kimataifa ambao unasifiwa na jumuiya ya kimataifa. Balozi wa Djibouti nchini China Bw. Abdallah Abdillahi Miguil anasema:

  "China inakabiliana na mgogoro huo wa afya ya umma kwa njia ipasavyo, hali ambayo imeonesha kuwa China ni nchi kubwa inayowajibika. Naamini kuwa China ina uhakika wa kushinda ugonjwa huo!"

  Sasa ni kipindi muhimu kwa China cha kupambana na ugonjwa. Aliyekuwa waziri mkuu wa Misri Bw. Essam Sharaf anasema:

  "Chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC na serikali ya China, wachina wote hakika watashinda ugonjwa huo, na China itakuwa na nguvu kubwa zaidi. Tunatarajia kuwa China itatoa mchango mkubwa zaidi katika kuhimiza dunia inatimiza kupata maendeleo yenye masikilizano."

  Mbali na hayo spika wa baraza la chini la bunge la Zimbabwe Bw. Jacob Mudenda alipokutana na balozi wa China nchini humo Bw. Guo Shaochun alisema, hali ya ugonjwa huo haitatingisha meli ya kiuchumi ya China inayosonga mbele. Zimbabwe inatumai kuimarisha ushirikiano na China katika sekta za afya, utalii, nishati endelevu na ujenzi wa maeneo maalumu ya kiuchumi. Pia kujifunza uzoefu wa utawala wa nchi, kuongeza urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili, na kuhimiza uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kupata maendeleo ya kina na yenye ufanisi zaidi.

  Urafiki wa dhati unathibitishwa wakati wa shida. Katika nusu karne iliyopita, China imepeleka timu ya madaktari elfu 21 barani Afrika, na siku zote inasimama bega kwa bega na Afrika katika kukabiliana na matishio mbalimbali ya usalama wa afya ya umma. Kama msomi wa Kenya alivyosema, baada ya mapambano hayo dhidi ya ugonjwa, urafiki kati ya China na Afrika utaimarishwa zaidi, Jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika itakuwa imara zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako