• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC yasisitiza usimamizi wa kazi ya kudhibiti maambukizi ya virusi

  (GMT+08:00) 2020-02-21 18:07:56

  Mkutano wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC umesisitiza usimamizi wa kazi ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona COVID-19 na utekelezaji wa dhati wa mkutano wa 4 wa wajumbe wote wa kamati hiyo, kupanga vizuri kazi ya ukaguzi wa nidhamu mwaka mzima, kufuata nidhamu kwa makini na kupambana na ufisadi.

  Mkutano huo umezitaka kamati za ukaguzi wa nidhamu za sehemu mbalimbali kuendelea kufanya ukaguzi na usimamizi kwenye kazi muhimu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya korona, na kuunganisha usimamizi na uhamasishaji ili kuwaongoza wanachama kufanya juhudi zote kutimiza jukumu hilo.

  Mkutano huo umesema mwaka huu ni mwaka muhimu wa kujenga jamii yenye maisha bora na kutokomeza umaskini. Kamati za ukaguzi wa nidhamu za sehemu mbalimbali zinatakiwa kuratibisha kazi ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi na kazi ya kuondoa umaskini, ili kutoa uhakikisho kwa kujenga jamii yenye maisha bora katika pande zote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako