• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uhusiano kati ya China na nchi za ASEAN waimarika zaidi kwa kupambana na virusi vya Korona kwa pamoja

  (GMT+08:00) 2020-02-21 18:08:59

  Mkutano maalumu wa mawaziri wa mambo ya nje wa China na Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia ASEAN kuhusu suala la viruvi vipya vya Korona COVID-19 jana umefanyika huko Vientiane nchini Laos.

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alifikia maafikiano muhimu kati ya China na nchi wanachama wa ASEAN kuhusu kushirikiana kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

  Hii ni mara ya kwanza kwa mawaziri wa mambo ya nje kufanya mkutano uliofuatilia usalama wa afya wa umma.

  Bw. Geng Shuang amesema, Bw. Wang Yi alieleza hatua na mafanikio ya China katika kupambana na virusi vya Korona, pia alitoa mapendekezo manne ya ushirikiano, ikiwemo kuimarisha umoja na kushirikiana kukinga na kudhibiti virusi hivyo, kufuatilia mustakabali na kuunda mfumo wa muda mrefu wa ushirikiano, kuvikabiliana virusi hivyo kwa msimamo wa kimantiki na kushinda hofu, na kutafuta fursa ya kufanya ushirikiano mpya kwa kutumia fursa hiyo ya kukabiliana na ugonjwa huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako