• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Nzige wavamia mashamba wilaya ya Bukwo Uganda

    (GMT+08:00) 2020-02-21 18:59:17

    Nzige wamevamia mashamba katika wilaya ya Bukwo katika mkoa mdogo wa Sebei nchini Uganda na kuharibu hekta kadhaa za chakula na mimea.

    Nzige waliingia wilayani humo Jumanne jioni kupitia kaunti ndogo ya Riwo, karibu na jimbo la Pokot Magharibi nchini Kenya.

    Ofisa Uzalishaji wa Wilaya ya Bukeni, Bwana Franklin Kitiyo, amesema nzige haohuenda ndio kundi kubwa zaidi kuwahi kuingia Uganda.

    Wadudu hao, ambao waliingia kwanza kupitia Wilaya ya Amudat mapema mwezi huu, wameenea hadi Moroto, Nabilatuk, Nakapiripirit, Napak, na Abim.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako