• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Mnada wa madini ya Almasi kufanyika Mwadui

    (GMT+08:00) 2020-02-21 18:59:56

    Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Wizara ya Madini, wanatarajia kufanya mnada wa madini ya almasi katika Mgodi wa Mwadui ulioko wilayani kishapu, kwa kuuza asilimia tano ya madini yaliyozalishwa na mgodi huo.

    Mkuu wa Mkoa huo, Zainab Telack, amesema Mkoa wa Shinyanga unakwenda kuweka historia kwa kufanya mnada wa madini hayo kwa mara ya kwanza, akibainisha kuwa serikali na mgodi walikubaliana asilimia tano ya madini yanayozalisha katika mgodi huo, yauzwe kwa wazawa ili nao wanufaike na rasilimali za nyumbani na kuinuka kiuchumi.

    Baadhi ya wafanyabiashara wa madini hayo, wamepongeza serikali kwa kupigania wazawa kunufaika na rasilimali za nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako