• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yawaunga mkono zaidi wahudumu wa afya wa kike wanaopambana na mlipuko wa korona

    (GMT+08:00) 2020-02-21 19:52:54

    China imeongeza juhudi kuwaunga mkono wahudumu wa afya wa kike wanaopambana na mlipuko wa virusi vya korona COVID-19, ikiwemo kuwapatia ushauri wa kisaikolojia na kusaidia familia zao.

    Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake wa China, ulio chini ya Shirikisho la Wanawake nchini China, limechanga dola za kimarekani 320,000 kuwasaidia wanawake hao walio mstari wa mbele katika kupambana na virusi vya korona, ikiwemo kuwanunulia taulo za wanawake.

    Mashirikisho ya wanawake katika maeneo wanakotokea wahudumu wao yamewasiliana na familia zao na kuwanunulia mahitaji ya lazima ya kila siku pamoja na kutoa msaada wa kisaikolojia. Pia wameandaa walimu wanaowafundisha watoto wao kupitia mtandao wa internet na kuanzisha makundi ya mawasiliano kupitia simu za mkononi ili kuwasomea vitabu watoto wadogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako