• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ajibu barua ya tajiri wa Marekani Bill Gates

    (GMT+08:00) 2020-02-22 19:12:36

    Rais Xi Jinping wa China amejibu barua ya mwenyekiti wa Mfuko wa Gates wa Marekani Bw. Bill Gates, na kumshukuru yeye na mfuko wake kwa kuunga mkono juhudi za China za kupambana na maambukizi ya virusi vipya vya korona COVID-19, na pia ameitaka jumuiya ya kimataifa iongeze uratibu na kupambana na maambukizi hayo kwa pamoja.

    Rais Xi amesema tangu mlipuko wa COVID-19 utokee, China imechukua hatua mbalimbali ambazo hazijawahi kuchukuliwa ili kupambana na ugonjwa huo, na kupata ufanisi mkubwa. Ameongeza kuwa serikali ya China inalinda kwa nia thabiti usalama na afya ya wananchi, na pia kujitahidi kutoa mchango kwa ajili ya usalama wa afya duniani.

    Aidha rais Xi amesema binadamu tuko kwenye jumuiya yenye hatma ya pamoja, na mshikamano ni silaha yenye nguvu zaidi katika kupambana na ugonjwa unaotishia usalama wa watu wote. Amesema anatumai kuwa jumuiya ya kimataifa itaongeza uratibu, na kufanya juhudi za pamoja kwa ajili ya afya na maisha bora ya binadamu wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako