• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika haipaswi kuchukuliwa na Marekani kuwa uwanja wa vita dhidi ya China

    (GMT+08:00) 2020-02-23 19:55:05

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo hivi karibuni alimaliza ziara nchini Senegal, Angola na Ethiopia na katika Umoja wa Afrika. Hii ni mara yake ya kwanza kufanya ziara katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa Sahara, katika karibu miaka miwili iliyopita, tangu ateuliwe kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

    Katika ziara hiyo, Pompeo alipohutubia mjini Addis Ababa, Ethiopia alizitaka nchi za Afrika "zikae macho na serikali inayolazimisha utii na ahadi zake za maneno matupu", na kusema uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na Marekani ndio njia ya Afrika ya "kujikomboa kiuhalisi". Japo hakuitaja China kwenye hotuba yake, lakini Shirika la Utangazaji la Marekani limesema, moja ya madhumuni muhimu ya ziara hiyo ya Pompeo ni kupunguza ushawishi wa uwekezaji wa China barani Afrika.

    Hivi sasa nchi za Afrika zinajitahidi kuharakisha mchakato wa maendeleo ya viwanda. Lakini hali duni ya miundombinu, na upungufu wa watu wenye uwezo na mitaji, vimekuwa kizuizi kikubwa katika kutimiza lengo hili. Takwimu zinaonesha kuwa, asilimia 20 ya uwekezaji kwenye miundombinu barani Afrika imetolewa na China, huku ule uliotolewa na Marekani ukiwa ni asilimia 1.7 tu. Kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2018 mjini Beijing, rais Xi Jinping wa China alitangaza "hatua nane" za kuimarisha ushirikiano na Afrika, ikiwemo kutoa nafasi nyingi zaidi kwa wanafunzi wa Afrika kusoma na kufanya mawasiliano ya elimu nchini China. Kutokana na takwimu zisizokamilika, mwaka jana wanafunzi wa Afrika wanaosoma nchini China wamefikia elfu 60, na China imekuwa nchi ya pili yenye wanafunzi wengi zaidi wa Afrika duniani baada ya Ufaransa. Wakati huohuo, mwanzoni mwa mwezi huu, rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kuzidishwa kwa kikwazo katika utoaji wa viza kwa watu wa nchi za Afrika, zikiwemo Nigeria, Sudan na Tanzania. Hatua hiyo itaathiri robo moja ya Waafrika wanaotaka kwenda Marekani. Kabla ya hapo, serikali ya Marekani imepunguza misaada na uungaji mkono wa kifedha kwa nchi za Afrika, na hata rais Trump alitukana nchi hizo ni kama "nchi za shimo la choo".

    Haki ya kujiendeleza ni haki ya kimsingi ya binadamu. Bara la Afrika lina nchi nyingi zaidi zinazoendelea, nia ya Waafrika ya kujiendeleza na kujiamulia njia ya kujiendeleza inapaswa kuheshimiwa na jumuiya ya kimataifa. Wakati wa vita baridi, Marekani ilizitaka nchi nyingine zichague kuwa katika upande wa Marekani au wa Urusi wa Kisovieti. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya hivi karibuni alipohojiwa na wanahabari wa Marekani alisema, mawazo ya vita baridi yamepitwa na wakati, nchi za Afrika hazipaswi kutatizwa tena na machaguo hayo.

    Serikali ya China kwa mara nyingi imesisitiza kufurahia ushirikiano wowote unaonufaisha uchumi, jamii na maisha ya watu barani Afrika. Mtafiti wa Taasisi ya Brookings mjini Washington Addisu Lashitew alisema, uwekezaji wa China barani Afrika ni safi sana, kama Marekani ikitaka kuwa mwenzi halisi wa Afrika, inatakiwa kuheshimu haki yake ya kuchagua wenzi wengine wa kufanya ushirikiano, ikiwemo China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako