• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mradi wa kujitolea kupambana na virusi vya korona mjini Wuhan wavutia zaidi ya watu elfu 10

  (GMT+08:00) 2020-02-24 10:01:40

  Mradi wa kujitolea umewavutia watu zaidi ya elfu 10 katika mji wa Wuhan, ambao ni kiini cha maambukizi ya virusi vipya ya korona vinavyosababisha nimonia (COVID-19), mkoani Hubei, China, muda mfupi tu baada kuanzishwa.

  Serikali ya huko imetangaza kuwaandikisha watu wanaojitolea kuwasaidia wakazi wa Wuhan ambao wanatakiwa kukaa nyumbani ikiwa sehemu ya hatua za kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo, kununua vyakula kwenye maeneo ya mjini.

  Ofisa wa mji huo Bw. Chen Qiangsheng amesema tangu ugonjwa huo ulipolipuka mjini humo, zaidi ya watu elfu 50 wamejitolea kufanya kazi mbalimbali kwenye mitaa ya makazi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako